African Rift Valley – SW

Read this page in English

Mpango wa Bonde la Ufa la Afrika unaunga mkono mashirika Asili na jumuiya ya ndani na jumuiya ya kiraia na juhudi zake shirikishi kwa marafiki wa kimaeneo, kitaifa na kimataifa ili kuimarisha maisha na kiwango cha mandhari endelevu. Mpango huo unalenga mandhari msingi mawili:

 • Jangwa la Mosaic la Kaskazini mwa Kenya: Nyumbani kwa makabila mengi zaidi ya watu wafugaji vile vile wavuvi na wawindaji ambao wamesimamia rasilimali asili ya mazingira haya ya jangwa kwa makazi.
 • Maeneo Tambarare ya Kusini na Nyanda za juu za Kusini mwa Ethiopia: Ufugaji mbalimbali wa ngo’mbe, mbuzi na kondoo unanawiri katika maeneo tambarare wakati baadhi ya mandhari ya ukulima ya zamani zaidi ya ulimwengu imeendelezwa katika maeneo ya miinuko.

Kuingia kwenye muongo wa pili wa uundaji ruzuku hapa. mpango wa Bonde la Ufa la Afrika unasaidia juhudi za kusimamia na kudumisha maisha yanayozingatia utamaduni kwenye shamba za mababu na kuiga mifumo ya usimamizi wa rasilimali yao kwa njia bunifu ambazo zinaimarisha uhuru na uhimili wa chakula. Bonde la Ufa la Afrika Mashariki limekuwa kama makazi muhimu ya bayoanuwai na jumuiya za binadam kwa miaka mingi zaidi. Ili kusaidia kuhakikisha kuwa eneo zinasalia sehemu maarufu ya mahusiano kati ya binadamu na tamaduni kwa vizaji vijavyo, tunalenga uundaji ruzuku wetu katika mandhari haya muhimu:

 • Uimarishaji uchumi asili na chaguo za maisha
 • Ukuzaji wa mifumo Asili ya kilimo cha ikolojia na mimea asili
 • Uimarishaji Taasisi Asili kwa usimamizi wa rasilimali asili
 • Kulinda njia za kitamaduni za uhamiaji na maeneo ya sherehe
 • Udumishaji wa amani katika mipaka na ushirikiano miongoni mwa jumuiya za wafugaji wa kuhamahama
 • Ukuzaji wa tamasha za utamaduni zinazoangazia miunganisho kati ya muziki, densi, vyakula, uhuru, amani na uhimili
 • Uungaji mkono vikundi vya jumuiya ili kudumisha na kuimarisha lugha na sherehe
 • Uungaji mkono wa utafutaji kwenye viungo kati ya maisha ya jadi, vyakula na mifumo ya uongozi na mabadiliko ya hali ya anga na uendelevu
 • Uungaji mkono elimu muhimu ya kitamaduni kulingana na maarifa ya jadi
 • Uendelezaji wa sera za usimamizi katika kiwango cha kitaifa, kimaeneo na kimataifa

Experiences